Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MWANASIASA mkongwe na maarufu nchini Tanzania mzee Kingunge Ngombale-Mwiru(87), amefariki dunia,akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Akizungumza na Michuzi Blog asubuhi hii kuhusu taarifa za kifo cha mzee Kingunge ,rafiki wa mkubwa na wakaribu wa mtoto wa Kinje, Abdull Nsembo amesema ni kweli amefariki saa 9:30 ya alfajiri ya leo akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
"Ni kweli mzee wetu amefariki saa 9:30 alfajiri ya kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu.Taarifa rasmi itatolea kuhusu taratibu nyingine lakini kwa sasa tunaendelea na kikao na kisha tutaufahamisha umma.

Kabla ya kukutwa na umauti Januari mwanzoni Mzee Kingunge alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa majeraha yaliyotokana na kuumbwa na mbwa nyumbani kwake na akafanyiwa upasuaji.
Hata hivyo wakati anaendelea kupatiwa matibabu,mke wake Peras alifariki dunia mwezi uliopita.
KINGUNGE MWANASIASA MWENYE HISTORIA
Mzee Kingunge enzi za uhai wake katika harakati zake za kisiasa alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu na miongoni wa watu waliokuwa na ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM).Ameitumikia CCM na Serikali kwa kipindi kirefu na miongoni mwa wanasiasa wenye historia ndefu nchini.
Pamoja na kuwa CCM kwa muda mrefu, wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Kingunge aliamua kuondoka CCM na kisha akatangaza kumuunga mkono Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye naye aliondoka CCM na kujiunga Chadema na kisha kupata fursa ya kuogombea urais akiwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa).
Wakati anaondoka CCM alitoa sababu nyingi lakini kubwa alidai kuwa kinachomuondoa aliona kuna ukiukwaji wa Katiba ya chama hicho.
ALIAHIDI KUTOHAMA CCM
Hata hivyo mzee Kingunge baada ya kujiweka kando na masuala ya kiasisa tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, alikuwa kimya na historia inaonesha kuwa amekuwa CCM tangu ilipoanzishwa mwaka 1977.
Kutokana na historia yake na CCM, siku za karibuni Rais ,Dk.John Magufuli alikwenda kumjulia hali mzee Kingunge alipokuwa amelazwa Muhimbili akiwa Wodi ya Mwaisela ambapo alitumia nafasi hiyo kumueleza Rais kuwa bado anaipenda sana CCM.
Kutokana na historia yake na CCM, siku za karibuni Rais ,Dk.John Magufuli alikwenda kumjulia hali mzee Kingunge alipokuwa amelazwa Muhimbili akiwa Wodi ya Mwaisela ambapo alitumia nafasi hiyo kumueleza Rais kuwa bado anaipenda sana CCM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...