Na Said Mwishehe,Blogu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema bado ni changamoto kwa watanzania walio wengi katika kutunza fedha za noti na noti ya sh.500 na noti ya Sh.1000.

Hayo yamesemwa leo mkoani Mtwara na Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu kutoka Benki Kuu Tanzania(BoT) Dolla Abdull wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari waliokuwa kwenye semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika taarifa sahihi za uchumi.

Akifafanua kuhusu fedha chakavu, amesema noti ya Sh.500 ndio inayochakaa zaidi ukilinganisha na noti nyingine inayofuata kwa kuchakaa ni ya Sh.1000.Amesema sababu ya fedha hizo kuchakaa haraka inatokana na kutumika zaidi kwenye mzunguko wa fedha hasa kwa kuzingatia kundi kubwa la wananchi ndio watumiaji wakubwa.

"Hii noti ya Sh.500 na ya Sh.1000 zinatumika zaidi ukilinganisha na noti ya sh 10,000. Ni fedha ambazo zipo kwenye mzunguko zaidi." Pia utunzaji wa fedha bado changamoto kubwa katika jamii na ndio maana zinachakaa mapema.Ukifuatilia zaidi utabaini hizi noti za Sh.500 wengi ambao wanazitumia hawazitunzi vizuri na wala haziwapeleki benki,"amesema Dolla.

Amefafanua sababu nyingine ya fedha hizo kuchakaa haraka inatokana na ukweli uliopo watanzania ambao wwnatunza fedha zao benki hawazidi asilimia 14.Hivyo amesema sehemu kubwa ya fedha inabaki mtaani na matokeo yake zinachakaa. "Ujue fedha nayo ina umri wake wa kuishi ambapo kwa fedha za noti ni zinaishi kati ya miezi sita hadi saba.

" Kazi yetu idara ya sarafu ni kuhakikisha tunapeleka fedha safi katika mzunguko na zile ambazo zimechakaa tunazisaga katika mashine maalumu,"amesema Dolla.

Ametoa ombi kwa Watanzania kuhakikisha wanatunza fedha hizo kwani Serikali inatumia gharama kubwa kuchapa fedha hizo huku akifafanua fedha ni moja ya alama ya nchi yetu,hivyo lazima zitunzwe vizuri.Amesititiza wananchi kutunza fedha zao benki kwani ni njia moja wapo ya kuzifanya fedha kuwa safi huku akiwakumbusha wenye fedha zilizochaa kuzipeleka benki ili zibadilishwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...