Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ninamshukuru sana Mzee Warioba kwa ufafanunizi wake. Mimi nilipojiunga kama mwanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1973 nilijiunga na TANU Youth League, tawi la Mlimani. TANU Youth League ilikuwa ni hivyo alivyotamka Mzee Warioba, kwamba tulikuwa na utayari wa kupingana na TANU na serikali ilipobidi. Kwa pale chuo kikuu, tulikuwa tunachapisha jarida lililoitwa "Maji Maji," ambalo lilifahamika hadi nje ya nchi. Tulikuwa tunachambua masuala, iwe ni ya mapinduzi nchini, ujamaa vijijini, siasa za mambo ya nchi za nje, ukombozi, na kadhalika. Vile vile, tulikuwa tunaendesha madarasa ya itikadi ("ideological classes") kila Jumapili, ambayo yalihusu mihadhara na mijadala juu ya masuala haya. Madarasa hayo yalikuwa yakivuma na kupendwa sana, sio tu na wanachuo bali pia watu wa mjini Dar es Salaam.

    Katika yote hayo, tulimwona Kingunge Ngombale Mwiru kama mtu wa kupigiwa mfano, kwa maana kwamba alikuwa ameiva kiitikadi. Akiwa mkuu wa chuo cha itikadi cha TANU Kivukoni, Ngombale Mwiru alifanya kazi kubwa ya kulea makada wa TANU. Chuo chake kilikuwa kinachapisha jarida lililoitwa "Mbioni." Baada ya kutangazwa "Azimio la Arusha," Ngombale Mwiru alichapisha uchambuzi wa "Azimio" katika jarida hilo. Ninavyokumbuka, huu ulikuwa ni uchambuzi wa mwanzo kabisa wa "Azimio la Arusha" kuchapishwa

    Kwa ujumla TANU Youth League pale Mililani tulikuwa na msimamo wa kushoto ("leftist") kuliko TANU. Yaani kwa ujumla, sisi tulishikilia mtazamo wa ki-Marxisti au "scientific socialism." TANU haikuenda mbali namna hiyo. Ilijikita katika ujamaa wa ki-Afrika. Mwalimu Nyerere alikuwa akija pale Mlimani kulumbana na wanachuo, na alitambua tofauti baina ya msimamo wake (na TANU) na msimamo wetu. Hata hivyo, alikuwa anasisitiza kuwa alitegemea vijana tuwe kushoto zaidi ya TANU na serikali yake.
    Huu ulikuwa msimamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu wanachuo kwa ujumla. Katika hotuba zake pale chuo kikuu kwetu wanachuo wote, alikuwa anatuambia kuwa hataki kuona chuo kinatoa wahitimu wa "ndio ndio." Kwa maana nyingine, alitaka tuwe watu wa kuhoji mambo.

    Kama alivyogusia Mzee Warioba, ninaona ni muhimu tuangalie hali ya leo kwa kufananisha na miaka ile. Mimi kwa uzoefu wangu ndani ya TANU Youth League nawajibika kusema neno kuhusu Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). UVCCM imepotea njia. Inajitangaza muda wote kwamba jukumu lake ni kutetea na kutekeleza maamuzi na mipango ya CCM. Nikizingatia kuwa UVCCM iko hadi vyuoni, nawajibika kusema kuwa msimamo huu ni msimamo potofu. Vyuoni ni mahali ambapo tunawajibika kutafakari mambo. Nilitegemea UVCCM vyuoni iwe ni chachu ya tafakari na kuchambua mambo kama tulivyokuwa tunafanya TANU Youth League, na iwe tayari kukosoa. Imetuangusha.

    ReplyDelete
  2. Nimeona kuwa ujumbe wangu mrefu hapa juu haukutambulisha jina langu lote. Basi najitambulisha vizuri ili wadau wafahamu kuwa mimi ndiye niliyeandika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...