Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Mhe.Selemani Jafo amewataka Wadau wote wa Elimu pamoja na jamii kwa
ujumla kushirikiana na serikali kutekeleza sera ya elimu Bila Malipo.
Jafo ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi vifaa vya shule katika shule ya msingi Uguzi, iliyopo wilayani Chamwino, mkoani Dodoma.
Vifaa hivyo vilitolewa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Dkt. Ombeni Msuya na Abdala Jacob kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.Amewataka wadau hao wasikate tamaa kuunga mkono Serikali kuhusu Elimu. “Japo changamoto ni nyingi lakini wanafunzi wenye uhitaji maalum wanahitaji msaada wao”. alisisitiza
Amesema wanafunzi wengi wanakosa fursa ya vitendea kazi kama madaftari na kalamu hivyo ni jambo la msingi kwa wadau wa elimu kuendelea kusaidia watoto hao na kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza sera ya Elimu Bila Malipo.
Waziri Jafo pia alizindua mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”. Waziri Jafo amesema ujumbe huo unamhusu mtoto mwenye uhitaji wa kupata elimu na kuwaomba Watanzania kwa ujumla kuunga mkono jambo hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalum wa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum ambao ameupa jina la “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo akikabidhi madaftari kwa wanafunzi na uzinduzi wa mpango wa “Nisaidie daftari na peni nami nipate elimu”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...