MKUUWAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa
viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba ambao wameahidi kununua pamba
yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.
Viongozi
hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw.
Hamza Rafiq Pardesi na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei ambao
kwa pamoja wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa.
Waziri
Mkuu amekutana na viongozi hao leo (Jumatatu, Februari 12, 2018) jijini
Dar es Salaam na amesema kwamba wakulima waliitikia wito wa Serikali wa
kufufua zao hilo, hivyo mwaka huu wanatarajia kupata mavuno mengi.
Waziri
Mkuu amewataka viongozi hao wajiandae kununua pamba nyingi kwa sababau
mwaka huu wakulima wamelima pamba ya kutosha baada ya Serikali
kuwahamasiha waongeze uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa viwanda vikubwa viwili vya kuchakata pamba cha Namera Group of Industries,na JOC. Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu huu.Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa JOC Bw. Qin Mengwei (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi (kushoto mwenye miwani nyeusi) . Wakurugenzi hao wameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini Tanzania. Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao leo, Februari 12, 2018 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. PICHA NA OFISI YA WAZIRI
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...