WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekamata meli ya uvuvi mali ya Kampuni ya Buah Naga 1 ya nchini Malaysia na kuitoza faini ya Dola za kimarekani 350,000 sawa na Sh.milioni 770 kwa kosa la kukutwa na mapezi ya samaki aina ya papa yenye uzito wa kilo 90 bila miili yake.

Ambapo hiyo ni kinyume cha Kanuni ya 66 ya kanuni za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.

Meli hiyo ilikamatwa Januari 26 mwaka huu baada ya kufanyika ukaguzi uliosimamiwa na kikosi maalum cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa samaki na mazao yake wakati ikifanya shughuli za uvuvi katika ukanda wa Bahari Kuu kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara.Pamoja na kukutwa na mapezi hayo ya papa, meli hiyo ilikutwa pia na bastola aina ya Bereta ikiwa na risasi 10 bila ya kuwa na nyaraka za umiliki wake.

Akizungumza mjini Mtwara ambako meli hiyo ndiko inakoshikiliwa na Serikali Waziri Mpina ameagiza fedha hizo zilipwe ndani ya siku saba huku akitoa onyo kali kwa wamiliki wa meli waliopewa leseni za uvuvi wa Bahari kuu kufuata masharti ya vibali vyao na katika zama hizi za utawala wa Rais, Dk.John Magufuli watachukuliwa hatua kali zaidi.

"Enzi za Serikali ya Awamu Tano ya Rais Magufuli mtakaguliwa na kupekuliwa kuliko wakati wowote, hivyo ni vizuri mkatii sheria za nchi kwa mujibu wa leseni zenu,"amesema Mpina huku akisilizwa na Kapteni wa meli hiyo Han Ming Chuan  raia wa Taiwan.

Mpina amesema meli hizo zimekuwa zikitumika pia kufadhili biashara nyingine haramu ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya ,usafirishaji haramu wa  binadamu na biashara ya silaha.Pia zinatumika kutorosha nyara za Serikali ikiwemo meno ya tembo, samaki na madini.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Francis Mkuti wakionesha baadhi ya Samaki waliovuliwa na Meli hiyo.
 Hosea Mbilonyi Kaim Mkurugenz mamlaka ya Usimamiz wa Bahari Kuu  DFSA akimuonesha waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina shehena ya Samaki  tani 4.5 wasiotakiwa kuvuliwa ambao wanatakiwa Kupigwa Mnada Siku Yoyote.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akilekea katika Meli Buah Naga one kukagua Samaki walivuliwa kinyume na Taratibu

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...