Na Agness Francis Globu ya jamii
Kikosi cha YangaSc Kilichoelekea Nchini Botswana katika mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers katika michuano inayoendelea ya Klabu Bingwa Afrika.
Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa kesho machi 17 mwaka huu huko Nchini Botswana.
Mchezo uliopita ambao ulichezwa Jijini Dar es Salaam uwanja wa Taifa wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo walicharazwa mabao 2-1.
Yanga anakabiriwa na kibarua kigumu ambapo anatakiwa kushinda magoli zaidi ya 2 kwa bila ili kuweza kupata tiketi ya kuendelea kusonga mbele katika hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika.
Mchezaji wa kikosi hicho Ibrahim Ajibu Migomba amesema kuwa matarajiao yao ni kuondoka na ushindi mnono huko ugenini ili kuendelea kusonga mbele zaidi.
"Tumedhamiria kuondoka na ushindi jumamosi ili tusonge mbele hatua ya makundi klabu bingwa Afrika Kikubwa dua na kudra za mwenyezi Mungu “amesema Ibrahim Ajibu.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...