Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem amezindua kituo cha kompyuta katika Shule ya Sekondari ya Old Tanga ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi huo unaofahamika kwa jila la “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”. kituo hiki ni cha pili kuzinduliwa nchini na Ubalozi huo kufuatia kile cha awali kilichozinduliwa mwaka jana katika Taasisi ya Taaluma Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Kituo cha Kompyuta katika Shule ya Old Tanga kimeunganishwa na huduma ya mtandao ili kuhamasisha wanafunzi juu ya matumizi ya teknolojia kwa kupitia kompyuta zinazopatikana ndani yake ili kufanikisha utekelezaji wa mipango ya elimu kwa njia za kieloktroniki.
Wakati huo huo Balozi Al-Najem amezindua uwanja wa mpira wa miguu,  mpira wa wavu na pia  kuahidi kusaidia na kugharamia ujenzi wa viwanja hivyo  kwa kubadilisha eneo ambalo lilikuwa limetelekezwa na kulifanya viwanja vya michezo.

Pia Balozi aligawa geloni za kuhifadhia maji za lita 22 kwa kila darasa katika Shule ya Sekondari ya Old Tanga kuwarahisishia wanafunzi kupata maji safi na salama badala ya kusongamana na kusukumana katika kisima ambacho kilizinduliwa na balozi miezi michache iliyopita.
 Hii ni ziara ya pili kufanywa na Balozi wa Kuwait katika Shule ya Sekondari ya Old Tanga baada ya ziara ya kwanza mwezi Desemba mwaka jana ambapo alizindua kisima ikiwa ni mwendelezo wa mradi wa Ubalozi “KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE” kwa ushirikiano na Taasisi ya Direct Aid ya Kuwait.
Katika ziara ya mwisho Balozi alifuatana na maafisa mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa Bodi ya Shule na meya wa zamani wa Tanga Bwana Salim Kisauyi, mkurugenzi wa jiji la Tanga na afisa elimu waliowakilishwa na afisa Taaluma Bhoke Robin na afisa elimu wa Kata Furaha Godfrey na mwakilishi wa Meya wa sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...