-Uzalishaji utapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa usambazaji kwa wateja.- Uzalishaji wa michanganyiko mbalimbali ya saruji utazingatia makubaliano ya ushuru.
- Kituo hicho kipya cha uzalishaji kitachochea huduma bora kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya BASF yenye ufumbuzi wa bidhaa bora.
Kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa kemikali duniani vilevile
kemikali za ujenzi , imeanza kuwekeza madhubuti kwenye uzalishaji wa
ndani na hivi leo imekabidhi kituo cha uzalishaji nchini Tanzania.
Kiwanda hicho ambacho kitazalisha mchanganyiko wa saruji, kitatumika
kupitia makubaliano maalum ya ushuru na kitatoa ufumbuzi wa kibunifu ili
kuiwezesha BASF kukidhi mahitaji ya wateja.
Kutokana na kiwanda hicho kipya, kitengo cha kemikali na ujenzi BASF kitajiimarisha katika wigo wa kuwafikia wateja wake wengi zaidi na kukidhi mahitaji ya soko huku ikitoa ufumbuzi wa hali ya juu katika sekta ya ujenzi. "Uwekezaji huu ni hatua nyingine muhimu kwa BASF Afrika.
Ushiriki wetu katika bara la Afrika unaongezeka na jukumu kubwa muhimu linalotekelezwa na kitengo hichi ni kutazama zaidi kwenye nchi zenye mipango mizuri na fursa kubwa, kama vile Tanzania "alisema Michael Gotsche, ambaye ni Makamu wa Rais wa BASF Afrika.
Christian Geierhaas ambaye ni Makamu wa Rais wa kitengo cha kemikali za ujenzi Upande wa Mashariki ya Kati, Asia Magharibi, CIS & Afrika, alisema kuwa "Kuwekeza nchini Tanzania, kutaiwezesha kitengo hicho kuleta bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu na ufumbuzi zaidi kwa wateja wetu katika soko hili muhimu."

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...