HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigamboni inatarajia kutumia zaidi ya bilioni 5 kwaajili ya ujenzi wa makao makuu ya Manispaa yanayojengwa eneo la Gezaulole katika manispaa hiyo mpya.

Akizungumza  wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya Manispaa hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, David Sukali na viongozi wa UVCCM Mkoa waliotembelea kuona hatua mradi  ilipofikia mwishoni mwa wiki amesema kuwa, ujenzi upo kwenye hatua za awali ambapo  Mkandarasi Tanzania Building Agency(TBA) Bridge ndiye aliyepewa tenda ya ukamilishaji wa jengo hilo.

Ameongeza kuwa jengo hilo linajengwa kwa kutumia gharama kutoka Serikali kuu na fedha za ndani za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Kaimu Mkurugenzi ameleza kuwa mradi utakapokamilika unatarajiwa kuwa na manufaa kwa watumishi wote wa Manispaa ya kigamboni, wakazi wote na  Wilaya jirani za Kigamboni na Serikali ya Jamhuri  ya Muungano  kwa ujumla.

Amesema kuwa mradi upo kwenye  hatua za awali za utekelezaji “mobilization and site clearance” ambapo  fedha  zilizotumika  mpaka  sasa ni Tshilingi.500,000,000/=.

Mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Manispaa ya Kigamboni ulianza Januari 2018 na unatarajiwa kumalizika Agosti 2018.

Viongozi wa UVCCM Mkoa walipongeza hatua zilizofikiwa na kusisitiza Mkandarasi kufanya kazi kwa juhudi ili kukamilisha mradi kwa wakati uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma bora.



Akifafanua kabla ya kuanza kutembelea miradi hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa yaa Kigamboni, David Sukali amesema kuwa miradi hii kutimiza irani ya chama cha mapinduzi ambazo ziliahidiwa katika uchaguzi wa mwaka 2015. 



Pia manispaa ya kigamboni inamradi wa kugawa pikipiki kwa kata za manispaa ya Kigamboni ambapo kila kata itapata pikipiki tano ambazo zitakuwa kwaajili ya vijana wa kata hizo kwaajili ya kujipatia kipato tofauti na wanavyoingia mikataba wanayoingia wanapata shida kubwa katika kikidhi mahitaji ya mikataba yao. 

Miradi ya Manispaa ya Kigamboni ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji, ujenzi wa barabara ya kwenda Daraja la Nyerere, ujenzi wa Ofisi za Manispaa hiyozzilizopo Gezaulole na ujenzi wa Zahanati. 

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa yaa Kigamboni, David Sukali akizungumza na umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Manispaa ya Kingamboni wakati wakielekea kwenye ukaguzi wa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Afya cha Kimbiji katika Manispaa ya Kigamboni pamoja na ofisi za Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam.

Mchumi wa Manispaa ya Kigamboni, Maximillian Manyuka akisoma matumizi  ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya cha Kimbiji, ofisi za Manispaa ya Kigamboni pamoja, ujenzi wa Zahanati pamoja na ujenzi wa barabara ya kuelekea daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala akizungumza na wafanyakazi wa Manispaa ya Kigamboni na baadae kueekea kukagua utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha afya cha Kimbiji, ujenzi wa barabara ya kuelekea Daraja la Nyerere, ujenzi wa Zahanati pamoja na ujenzi wa ofisi za Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, David Sukali (Mwenye suti ya  Bluu) akitoa maelekezo  kwa vijana wa  Mkoa wa Dar es  salaam na Viongozi wa vijana wa Manispaa ya Kigamboni katika Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji katika Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam
 Ujenzi ukiendelea katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha afya cha Kimbiji katika manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam,Musa Kilakala  akisaidiana na Wajenzi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji kutandaza nondo katika ujenzi wa kiuo hicho.
 Viongozi wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Temeke akitembelea kwenye mradi wa ujenzi wa Ofisi za Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Msanifu Majengo, Edwin Mwangasa(Mwenye tishet Nyekundu)Akitoa maelezo jinsi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Manispaa ya Kigamboni utakavyo kamilika pamoja na changamoto zinazomkabiri mhandisi huyo.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala  akisaidiana na mafundi kuweka nondo katika ujenzi wa ofisi za Manispaa ya Kigamboni.
Uonekano wa Majengo ya Ofisi za Manispaa ya Kigamboni zitakapokamilika hapo baadae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ninawapongeza sana Kari Nzuri,ujenzi upo yatua gani kwa sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...