BENDI
kongwe ya muziki wa dansi hapa nchini, The African Stars Twanga Pepeta,
inatarajiwa kuonyeshana ubabe na msanii wa muziki wa singeli anayetamba
nchini, Suleiman Jabir 'Msaga Sumu' katika shoo ya uzinduzi wa ligi ya
Handeni Kwetu Cup, utakaofanyika Machi 24, katika Uwanja wa Mkata,
wilayani Handeni, mkoani Tanga kuanzia asubuhi hadi jioni
itakapomalizika mechi ya ufunguzi ya mpira wa miguu.
Ligi hiyo inayoratibiwa na Kambi Mbwana kwa kushirikiana na Chama Cha Soka wilayani Handeni (HDFA), inasubiriwa kwa hamu na wadau wa michezo na burudani katika viwanja mbalimbali vya Kata wilayani Handeni, ambapo mbali na Twanga Pepeta na Msaga Sumu, wasanii wengine watakaotumbuiza ni Nyota wa Bongo Fleva, Top C, Bendi ya Handeni Super Makoba, wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa Handeni na vikundi vya burudani vya asili.

Akizungumzia tukio hilo, Mbwana ambaye pia ni mdau wa maendeleo wilayani Handeni, alisema uzinduzi huo utaweka historia kutokana na mikakati kabambe ya kuhakikisha kwamba mashabiki wanapata kitu kizuri kutoka kwa wasanii na wacheza soka kwa ujumla.
"Bendi ya Twanga Pepeta itakuwa na ziara Tanga Mjini kuanzia Machi 23 katika Ukumbi wa Tanga Hotel na Machi 24 usiku katika ukumbi wa Rombo Hotel, hivyo tumewaomba wakitoka Tanga, wapitie uwanjani Mkata ili wawape burudani ya dansi kwenye uzinduzi huo ambapo wameridhia.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...