Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma imejipanga kupambana na kutokomeza mimba za utotoni katika Wilaya hiyo.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kapeni ya Kutokomeza Mimba za Utotoni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Kata ya Haneti Wilayani Chamwino Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali amesema kuwa Kata yake na Wilaya kwa ujumla wamejipanga katika kupambana na vitendo vya ukatilia wa kijinsia yakiwemo matukio ya mimba na ndoa za utotoni .
Mhe. Peter Elia Chidawali ameongeza kuwa hawatakubali kuona watoto wao wanapoteza haki yao ya msingi ya kuendelezwa ya kupata Elimu kwa kupata mimba au kuolewa wakiwa bado shuleni.“Tutaendeleza Kampeni katika ngazi za familia kwa kuwaelimisha wazazi na walezi kuhusu madhara ya mimba za utotoni ili tuokoe kizazi cha kesho”alisema Mhe. Chidawali.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja amesema kuwa suala la mimba za utotoni limezidi kuongeza siku hadi siku hivyo basi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alizindua Kampeni ya Kutokomeza Mimba za utotoni kwa lengo la kuwezesha utoaji wa elimu kwa wanafunzi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushiriki mapambano dhidi tatizo hili.
Diwani wa Kata ya Haneti Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Peter Elia Chidawali akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo ‘Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima’ Wilayani Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja akitambulisha Kampeni ya Kitaifa ya Kuzuia Mimba za Utotoni kwa wanafunzi wa shule sambamba na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatil idhidi ya Wanawake na watoto katika Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala akiwaasa watoto wa kike kujitambua na kujilinda dhidi ya mimba za utotoni ili kupata haki ya kuendelezwa na kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia mimba za utotoni Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisikiliza ushauri wa malezi na makuzi kutoka kwa wataalamu jinsia ili kuwawezesha kupambana na mimba za utotoni wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...