Na Veronica Simba – Kigoma 

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, amesema kwamba ikiwa wananchi wa Kigoma watatumia vyema fursa za upatikanaji wa Madini ya Chumvi na Chokaa, zilizopo katika Mkoa huo, wanaweza kutajirika. 

Akihitimisha ziara yake katika Mkoa huo, jana Machi 3, baada ya kutembelea Migodi mbalimbali ya Madini ya Chokaa na Chumvi, Nyongo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa upatikanaji wa Chumvi na Chokaa ni neema kwa wananchi hao kutokana na uhitaji wake mkubwa katika maisha ya kila siku. 

“Ni fursa kubwa sana kwa wananchi wa Kigoma. Wasidhani kwamba fursa iliyopo hapa ni ya uvuvi na mawese peke yake; wanaweza kuwa matajiri wakubwa kupitia Madini ya Chokaa na Chumvi.” 

Akifafanua zaidi, Nyongo alisema kuwa, katika siku mbili za ziara yake mkoani Kigoma, ameshuhudia maeneo mengi yenye Chokaa ya kutosha na kwamba uzalishaji wake ni rahisi sana kwani kinachohitajika ni kuyachoma mawe husika na kusaga; basi. 

Akizungumzia upande wa Chumvi, alisema kuwa, Mgodi wa kuzalisha Chumvi wa Nyanza, uliopo Uvinza unafanya kazi nzuri katika uzalishaji lakini kwa bahati mbaya asilimia 70 ya bidhaa wanayozalisha, huiuza nje ya nchi hususan katika nchi jirani za Kongo na Burundi. 
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Ujumbe wake, akikagua maeneo mbalimbali ya Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), wakati wa ziara yake ya kazi mkoani Kigoma, Machi 3 Mwaka huu. 
Mmoja wa wafanyakazi katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza, ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mines), akifunga Mifuko ya Chumvi tayari kupelekwa Sokoni kwa ajili ya kuuzwa. Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), Mgodini hapo, Machi 3 Mwaka huu.
Shughuli za uchakataji chumvi zikiendelea katika Mgodi wa Chumvi wa Nyanza ulioko Uvinza (Nyanza Salt Mine), siku Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani), alipotembelea Mgodi huo akiwa katika ziara ya kazi, Machi 3 Mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...