Na Agness Francis Blogu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni  Dar es Salaam Ally Hapi amewaagiza watendaji wake kuhakikisha hadi ifikapo Juni mwaka huu wawe tayari wametoa fedha za mkopo Sh.bilioni 2.3 kwa wajasiriamali ambao ndio walengwa wa fedha hizo na kama itakuwa bado ataifumua idara ya maendeleo ya jamii.

Hapi ametoa maagizo hayo leo wilayani Kinondoni jijini wakati anazugumza kikao kati yake, wajasiriamali wa wilaya hiyo pamoja na watendaji ambapo la kikao hicho ilikuwa ni kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili 

Baada ya kusikiliza changamoto za wajasiriamali hao ,Hapi amesema moja ya changamoto ambayo imejitokeza kutofika kwa fedha Sh.bilioni 2.3 kwa wajasiriamali hao.

Amesema kama watendaji hao kazi imewashinda waondoke mara moja kuliko kutowatendea haki wajasiriamali kwa kuchelewesha fedha hizo hadi sasa bila sababu yoyote ya msingi. 

DC Hapi amesema Februari mwaka huu  ilitolewa Sh.bilioni 2.3 kwa ajili ya kukopeshwa vijana wajasiriamali ili kupanua biashara na kuendeleza pato la nchi.

"Nawahakikishia wakazi wa Kinondoni ikifikapo Juni mwaka huu fedha hiyo ikiwa haijafika kwa walengwa nitafumua idara yote ya maendeleo ya jamii.Hatutaki watu wasiofanya kazi kwa bidii,"amesema.

Aidha Hapi amesema ili kuondokana na Taifa la kuwa omba omba ni lazima kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kuongeza bila nguvu za wananchi Rais peke yake hataweza.
 Mkuu wa wilaya wa Halmashauri ya Kinondoni Ally Hapi akizungumza na wajasiriamali  wa wilaya hiyo wakati wa mkutano ambapo amewataka watoe kero na changamoto zinazowakabili ili kuzifanyia ufumbuzi leo katika ukumbi wa King Solomon Jijini Dar es Salaam.
 Afisa maendeleo ya Jamii  kata ya Ndugumi Halmashauri ya Kinondoni, Zuwena Mtani akifafanua jinsi ya kufanya kwa wajasiriamali hao ili kuweza kupata mikopo hiyo leo katika ukumbi wa King Solomon Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajasiriamali waliojitokeza kwa wingi katika mkutano leo ukumbi wa King Solomon  Jijini Dar es Salaam kutoa kero na changamoto zinazowakabili kwa DC Hapi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...