Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam  kupitia Umoja wa Rudisha uzalendo Tanzania (RUTA) umepongeza juhudi za Rais Dk.John Magufuli na watendaji kazi wake katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini huku wakitangaza kufanya maandamano ya amani Aprili 12 mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo na Mratibu wa umoja huo Charles Masele amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wananchi wengi wamevutiwa na wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli, hivyo katika kumpongeza wameandaa maandamano ya amani yatayohusisha watu wa itikadi zote yatakayofanyika Aprili 12 mwaka huu kuanzia Karume hadi viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa moja hadi saa tano asubuhi .

Wakizungumza zaidi  wadau hao wamesema hawana budi kuunga mkono juhudi za Rais kwani huduma nyingi zimeboreshwa zikiwemo miundombinu, afya hasa kwa akina mama na elimu ambayo hutolewa bure, pia mikopo ya elimu ya juu ambayo hutolewa kwa wanafunzi wa hali ya chini.

Aidha wameeleza utiifu wa Rais na watendaji wake wa serikali na taasisi binafsi kwa namna wanavyothamini na kuhudumu kwa haki na usawa hivyo wameona na vyema kumuunga mkono na kumuombea.

Pia umoja huo umewataka vijana na watu wa kada mbalimbali kuunga mkono juhudi hizo kwani zinafanywa kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na baadaye.
 Mratibu wa Umoja wa Rudisha Uzalendo Tanzania (RUTA), Charles Masele  akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandamano ya amani yatayohusisha watu wa itikadi zote yanayotarajia kufanyika Aprili 12 April mwaka huu, Picha na Emmanuel Massaa, Globu ya jamii,
Mratibu wa umoja huo,Charles Masele akifafanua jambo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...