NA JOEL MADUKA-GEITA.
Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGM) pamoja na Halmashauri mbili za Wilaya na Mji wa Geita zimetia saini ya Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja kuhusu Matumizi ya fedha za Huduma za Jamii zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa mwaka 2018.
Saini ya Makubaliano hayo inafuatia kutokana na marekebisho ya Sheria Mpya ya Madini iliyopitishwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kufanya mageuzi kwenye utekelezaji wa Fedha za Miradi ya Huduma za Jamii baina ya Kampuni za Uchimbaji Madini na Jamii kwenye eneo husika.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema Serikali mkoani humo imekusudia kuanzisha miradi mipya ikiwemo kiwanda cha sukari kutokana na mapato yanayotolewa na mgodi wa dhahabu wa GGM baada ya kuingia mkataba upya na halmashauri ya mji na wilaya ya Geita.
Aliongeza kuwa fedha zilizokwisha kutolewa na GGM kwa mwaka huu ni Bilioni tisa pointi mbili (B 9.2) ambapo fedha hizo zitatumika kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wawezesha wananchi kujikwamua na umasikini, ikiwemo kiwanda cha sukari ,afya elimu na mazingira.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi wakikabiana hati ya makubaliano ya miradi ya jamii na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso baada ya zoezi la Saini ya Makubaliano.
Wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri mbili ya mji na wilaya ya Geita wakisaini makubaliano.(katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi aweka saini kwenye hati ya makubaliano ya miradi kwenye halmashauri mbili ya mji na wilaya.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...