Taxify imetangaza punguzo la asilimia 50 kwa bei ya bajaji zake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuwavutia watumiaji wa huduma hiyo na kuwapa nafasi ya kutumia huduma zake.

Kampuni hiyo inayokuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika kupitia huduma zake mbalimbali za usafirishaji kwa kutumia teknolojia, imetangaza punguzo la asilimia 50 kuanzia Februari 28 kwa watumiaji wa Application yake ya ‘Taxify Bajaji’ ambapo wateja watalipa Shilingi 150 kwa kilometa na Shilingi 50 kwa dakika huku nauli ya kuanzia safari ikiwa Shilingi 300 kuanzia Jumatano Februari 28. Gharama ya nauli ya chini kabisa ikiwa Shilingi 1,000.

Wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya ya Usafir wa Bajaji kwa kutumia teknolojia wiki mbili zilizopita Taxify ilikuwa ikitoza malipo ya Shilingi 350 kwa kilomita, Shilingi 75 kwa kila dakika inayotumiwa katika safari, pamoja nauli ya chini ya shilingi 750.

"Punguzo la asilimia 50 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani kwa wale wote wanaopenda kutumia usafiri huu kwa safari fupi mjini ni hatua kubwa," alisema Remmy Eseka, Meneja Uendeshaji Taxify Tanzania.

Eseka alifafanua jinsi ambavyo watumiaji wa huduma hiyo watakavyokuwa wakilipa nauli zao pindi wanapofanya safari zao katika baadhi ya maeneo maarufu jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa kwa ofa ya punguzo la asilimia 50. "Huduma mpya ya Taxify Bajaji itatoza Shilingi 1,400 tu kutoka Makumbusho kwenda Sinza, Shilingi 1,800 kutoka Ubungo kwenda Mwenge na Shilingi 2,500 kutoka Tangi Bovu kwenda Mlimani City" alisema Eseka.

Akijibu swali, kuhusu mabadiliko ya bei iwapo kama yatawaathiri madereva wa bajaji wanaofanya kazi hiyo jijini hapa. Eseka alisema, "Tutawafidia madereva kwa kuwapa bonasi ili kuhakikisha kipato chao kinabaki kuwa kizuri, hivyo hawataathirika na punguzo hili la bei."

Taxify imeendelea kuwa maarufu jijini Dar es Salaam ikiwa ni miezi mitatu tu sasa tangu kampuni hiyo tanzu ya Estonia izunduliwe jijini hapa, lakini hadi sasa imekwisha zindua huduma zake mbili jijini Dar es salaam ambazo zipo katika programu za usafiri za Kampuni hiyo, kitu ambacho ni kinawafanya waweze kuongoza katika ushindani na kuwa kampuni ya usafirishaji kwa mtandao inayopendwa katika soko na wateja wake. 

Pia bei za sasa za huduma ya Usafiri wa Taxi kupitia programu ya Taxify zina punguzo la asilimia 25, huku nauli kwa kilometa ikiwa ni Shilingi 560, Shilingi 110 kwa dakika na nauli ya kuanzia Safari ikiwa ni kiasi cha Shilingi 1,200 na bei ya chini ya Safari ikiwa ni Shilingi 3,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. taxify ni wezi mimi na rafiki angu tumeshaibiwa na mmoja wa dereva wao, tuliacha mzigo na chenji chakushangaza yule dereva alitukimbia tukimpigia anakata simu tukibadilisha namba tukipiga inapokelewa tukijitambulisha sisi ni watu fulani anakata simu, tukamripoti ofisini kwao hakuna hatua yeyote iliyochuliwa mzigo hatukuupata na chenji haikurudi hadi kesho...

    Hivyo tumeamua kuachana nao na kubakia na rekodi yao hii mbaya ya kudeal na wateja wake, kikubwa tu tumeapa kutotumia tena usafiri wa Taxify huku tukiendelea kutoa ushuhuda kwa ndugu jamaa na marafiki juu ya tukio hilo baya la kukosa uaminifu kwa kiasi kikubwa namna hiyo.


    Bora uber, taxfy madereva hawana uaminifu


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...