
Na Bashir Nkoromo, Kigamboni.
Wanawake wajasiariliamali wametakiwa kutengeneza au kuuza bidhaa zenya ubora wa viwango vinavokubalika ili kuvutia wateja kununua bidhaa zao na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Dege katika Kata hiyo Angela alisema mbali na na bidhaa bora kuhamasisha wanunuzi na kuongeza masoko ndani na nje ya Nchi boa bidhaa hizo zinaweza kumudu ushindani katika soko.
Alivishauri vikundi vya Wanawake wajasiriamali kwenda kuomba mikopo kwenye Benki ya Wanawake Tanzania ambayo alisema ni benki yenye mikopo ya riba nafuu.
Uzinduzi wa Jukwaa hilo ni sehemu ya shamrashamra za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yatafanyika mapema mwezi huu.
Wanawake wa vikundi vya Wajasiriamali wakiandamana kutoka kwenye Ofisi yao kwenda kwenye uwanja wa Dege, kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Dar es Salaam, leo
Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akisoma moja ya mabango waliyokuwa nayo Wanawake Wajasiliamali walipowasili Uwanjani kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila.
Angel Akilimali akitazama mkeka uliotengenezwa na Mwanamke Mjasiriamali Jawa Maulidi (kushoto)
Angel Akilimali (kushoto) akimuuliza Mwanamke Mjasiriamali jinsi anavyotengeneza bidhaa zake.
Angel Akilimali na Diwani Chichi wakinywa togwa kwenye banda la maonyesho la Mwanamke Mjasiriamali, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...