KAMPUNI  ya Jumia Tanzania  inayojishughulisha na huduma za uuzaji na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia mtandao imemtambulisha Zadok Prescott kuwa Mkurugenzi Mkuu wake mpya.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wake uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Prescott alibainisha ni fursa kwake kujiunga na kampuni hiyo.

Ambapo amesema Jumia ni kampuni ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.

“Jumia ilianzishwa mnamo mwaka 2012 ikiwa na imani thabiti ya kwamba: ‘Mtandao wa intaneti unaweza kuboresha maisha ya Waafrika.’  "Ni vigumu kupata bidhaa unayoihitaji kupitia mfumo wa sasa wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali Tanzania.

" Upatikanaji wa bidhaa katika sehemu tofauti huwalazimu wateja kusafiri umbali mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kuongezea, bei hutofautiana kwa kila mfanyabiashara jambo linalosababisha kuwa ni changamoto kutambua kama unauziwa bidhaa kwa bei sahihi au la,"amesema.

Ameongeza ni  mfumo ambao humpotezea mteja muda na gharama katika maisha yake ya kila siku. Hivyo dhumuni kubwa la Jumia ni kuufanyia mabadiliko mfumo huo na kuufanya uwe wenye tija kwa wafanyabiashara nchini na kuwapatia wigo zaidi,” alisema Prescott.
 Mkurugenzi Mkuu mpya wa KAMPUNI  ya Jumia Tanzania,Zadok Prescott akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akijitambulisha na kueleza mikakati mipya ya kuiendelea kampuni hiyo ambayo kwa sasa imezidi kutanuka kila kukicha,kushoto kwake ni Meneja Masoko Albanny Jamess
Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albanny Jamess akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,kuhusu ujio wa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo,na kuelezea namna Jumia ilivyodhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...