Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Murad SadickA (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Bw. Emmanuel Lwehaula wakati wa ziara ya kutembelea mgodi wa Sekenke one Mkoani Singida.
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiangalia zoezi la uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki mara baada ya kutembelea mgodi wa Sekenke one Mkoani Singida.
Sehemu ya wachimbaji wadogo wadogo wa Sekenke one wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola (hayupo pichani) alipopata fursa ya kuzungumza nao na kusisitiza suala la usafi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akifafanua vifungu vya Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kwa watendaji wa Wilaya ya Iramba na kuwataka kuisimamia ili kudhibiti vitendo vya uchafuzi wa Mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akisalimiana na Bw. Dotto Roman Selasini Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Iramba mara baada ya kuwasili katika Mgodi wa Senkenke One ulipo katika Kijiji cha Nkonkilangi, Kata ya Ntwike, Tarafa ya Shelui, Wilaya ya Iramba akiongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kutembelea mgodi huo kwa lengo la kujionea hali ya mazingira mgodini hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...