NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .
SEKTA ya
Utalii nchini imepata suluhu ya Changamoto ya muda mrefu ya utoaji wa msaada wa
kitabibu, utafutaji na uokoaji wa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda
Mlima Kilimanjaro na Meru .
Changamoto
hiyo inafika kikomo rasmi baada ya kampuni ya
Kilimanjaro SAR kuzindua Kliniki ya kwanza Afrika ya magonjwa yatokanayo na
muinuko wa juu pamoja na utumiaji wa Helkopta kwa ajili ya uokoaji katika
Hifadhi za Mlima Kilimanjarona Mlima Meru.
Mbali na uzinduzi huo Kilimanjaro
SAR imeingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi ,kuanza kutoa
huduma za kitabibu kwa wagonjwa watakao pata matatizo wakati wa kupanda Milima
hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya
utiaji saini wa makubaliano kati ya Kampuni ya Kilimanjaro SAR na Hospitali ya
St Joseph ,Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba aliyekuwa mgeni rasmi amesema
hii ni fursa mpya kwa sekta ya Utalii kuutangaza vyema Mlima Kilimanjaro.
Huduma hii ya kwanza kutolewa barani Afrika inaiweka Tanzania katika
nafasi ya pili katika Ramani ya Dunia, kuwa na kliniki ya kipekee
katika utoaji wa huduma kwa wapanda Mlima na kwamba kwa kiasi kikubwa itasaidia
katika kuongeza idadi ya Watalii.
Hata hivyo
kuanza kwa huduma hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini ,bado ipo changamoto
ya matumizi ya uwanja mdogo wa ndege wa Moshi hali inayowalazimu kutumia uwanja
wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).
Ulbanie
Lyimo ni mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph akaeleza faida
itakayopatikana kutokana na kuingia makubaliano na kampuni hiyo ya Uokoaji ya
Kilimanjaro SAR kuongeza maarifa katika utoaji wa matibabu kutoka kwa madaktari
wa kigeni watakao hudumia wagonjwa wa Mlimani.
Kuanza kwa
kliniki hii ni msaada kwa maiha ya wapandaji wa Mlima Kilimanjaro na Meru
ikizingatiwa asilimia 75 ya magonjwa uwapo mlimani yanatokana na mbadiliko ya
Hali ya Hewa kulingana na urefu wa Mlima.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun akitia saini makubaliano ya Mashirikiano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi kuhusu uanzishwaji wa Kliniki ya utoaji matibabu kwa Wagonjwa wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru,kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister ,Urbanie Lyimo huku zoezi hilo likishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (aliyesimama kulia) ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR,Amour Abdallah.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo,Kippi Warioba na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji saini .




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...