Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Kampuni za bima nchini zimeshauriwa kuwahudua wananchi kwa uwazi na kutoa huduma za kiwango cha juu ili kuweza kuleta maendeleo ya kiuchumi.
Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba wakati mkutano wa wadau bima ulioandaliwa African Insurance Digital Banking uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa bima imeanzishwa kwa ajili ya kulinda biashara na mali hivyo wananchi wanatakiwa kuhudumiwa katika kulinda biashara na mali zao huku wakitoa elimu kwa uwazi.
Aliongeza kuwa mtu mwenye bima katika biashara au mali likitokea janga haiwezi kuwa sifuri kutokana na kukata bima kwa ajili ya biashara na mali hizo.
"Kampuni za Bima ili ziweze kufanya kazi ni lazima zisajiliwe katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi," alisema.
Alisema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda sekta ya bima zina mchango mkubwa katika kuwahudumia wananchi.
Nae Mwenyekiti wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.
Mwenyekiti
wa African Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu alisema kuwa
wameandaa mkutano katika kuweza kuwakutanisha wadau ikiwa ni kujenga
mtandao katika kutoa huduma na elimu ya bima kwa wananchi.
Mkurugenzi
wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea
mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima
yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Mkurugenzi
wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea
mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima
yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Mkurugenzi
wa Usimamizi na Ukaguzi wa Soko kutoka TIRA Bw. Elia Kajiba akitembelea
mabanda kujionea huduma zinazotolewa na makampuni ya bima
yaliyohudhuria maonyesho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...