Kufuatia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kutafuta wawekezaji wa Kimataifa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta utalii hapa nchini, Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China imejitokeza kwa lengo la kuwekeza katika utoaji wa huduma za kitalii zenye ladha na mandhari ya Kichina.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Tony, amesema kampuni hiyo imepanga kujenga hoteli za kitalii za kichina katika mji wa Karatu jijini Arusha na Serengeti mkoani Mara.

Akizungumza na Waziri wa Maliasil na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ofisini kwake mjini hapa jana kwa ajili ya kutambulisha mradi huo, Tony alisema mradi huo ni mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii wa China wanaotembelea Tanzania.

Alisema kupitia mradi huo jumla ya magari 500 ya safari  za utalii yatanunuliwa (Safari Cars) kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii hao wakati wa kutembelea maeneo ya vivutio hapa nchini.Pamoja na magari hayo alisema kampuni hiyo pia imepanga kuanzisha safari za moja kwa moja za ndege kutoka China hadi Tanzania ili kupunguza muda wa usafiri na gharama.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
 Wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Kigwangalla ofisini kwake mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi flash yenye picha za wanyamapori wa Tanzania Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing, aliyefahamika kwa jina moja la Tony kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza hapa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
 Waziri Kigwangalla akiendelea na mazungumzo na wakezaji hao.Na Hamza Temba - WMU-Dodoma.

HABARI ZAIDI  BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...