Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza mapema jana mbele
ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar kuhusiana na
maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018 litakalofanyika kwenye uwanja wa
CCM Kirumba Aprili 1 Jijini Mwanza na Aprili 2 Uwanja wa Halmashauri
mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Msama
ameanza kuwatangaza baadhi ya waimbaji watakaoshiriki tamasha hilo
ambalo limekuwa likiwavutia waimbaji wengi kila linapoanza kuandaliwa na
hatimaye kukamilika,Msama amemtaja mwimbaji mahiri jukwaani Boniface
Mwaiteje,Christina Shusho,Rose Muhando ambaye atazindua albamu yake mpya
siku hiyo, na wengineo ambao wanaendelea kujiunga kuhakikisha tamasha
hilo linafana. Pichani kulia ni mwimbaji Paul Clement pamoja na Beatrice
Mwaipaja,ambao walitambulishwa rasmi hapo jana.
Beatrice
Mwaipaja akifafanua zaidi namna ambayo ananendelea kujiandaa na
maandalizi yake tayari kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka
Kanda ya Ziwa kushoto ni Mwimbaji mwenzake Paul Clement.
Mwimbaji
Paul Clement akizungumza kuhusu maandalizi yake tayari kwa ajili ya
kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka Kanda ya Ziwa, kulia ni Mwimbaji
mwenzake Beatrice Mwaipaja .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...