Masako
amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia
burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka
sasa wamethibitisha kushiriki kwao.
Maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2018 yameendelea kunoga huku waimbaji mbali mbali wakiendelea kutambulishwa.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, RainFred Masako wakati akimtambulisha mwimbaji wa nyimbo za injili Martha Baraka.
Masako amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kujipatia burudani ya muziki wa njili kutoka kwa waimbaji mbali mbali ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki kwao.
Kwa upande wake mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Martha Baraka amesema kuwa yupo tayari kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kwa vile amejiandaa vyema."Tunaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa mjitokeze kwa wingi kuhudhuria Tamasha hilo ambalo nitaungana na waimbaji wenzangu kutoa burudani ya kukata na shoka," amesema Martha Baraka.
Tamasha hili linatarajiwa kufanyika Aprili 1-2, 2018 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Uwanja wa Halmashauri mkoani Simiyu,ambapo Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili Rose Muhando atazindua albamu yake mpya.
Waimbaji ambao mpaka sasa wamethibitisha kushiriki ni Christopher Mwahangila, Jessica BM Honore. Wengini ni Solomoni Mukubwwa, Danny M- Kenya na Ephraim Sekeleti.

Mmoja
wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili Martha Baraka akieleza namna
alivyojiandaa katika tamasha la pasaka 2018,mapema leo mbele ya
Waandishi wa habari (hawapo pichani).Kushoto ni Meneja wa Msama
Promotions Ltd,Jimmy Charles

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...