Na Paschal Dotto-MAELEZO   
         
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe. Benjamin William Mkapa ametangaza uteuzi wa  Profesa Egid Beatus Mubofu kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Idris Suleiman Kikula.

Uteuzi huo umetangazwa rasmi leo tarehe 5, Machi 2018 kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi   ya Mkuu wa UDOM, Mhe. Benjamin Mkapa.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Mubofu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kabla ya hapo alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Profesa Mubofu unaanza rasmi tarehe 17 Machi, 2018.

Profesa Idris Kikula ni miongoni mwa wanazuoni waandamizi wanaoheshimika ndani  na nje ya nchi kitaaluma kwa kushiriki katika tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii

Ameshiriki katika tafiti hizo kwa kushirikiana na taasisi nguli za kitafiti hapa nchini  kama REPOA, pamoja na taasisi ya UONGOZI.

UDOM ndio chuo kikuu pekee chenye uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi hapa nchini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na inakadiriwa kina uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban 40,000, pia kina eneo la ukubwa wa hekari zaidi ya 6000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mkuu check vizuri hiyo habari na picha. nadhani hiyo picha siyo ya Prof Mubofu aliyekuwa TBS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...