Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia) akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Dodoma, alipowatembelea akiwa katika ziara ya kazi, Machi 22 mwaka huu.
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akisalimiana na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Dodoma, alipowasili katika Ofisi hiyo akiwa katika ziara ya kazi, Machi 22 mwaka huu.
Shughuli za uchimbaji madini ya nakshi zikiendelea katika Mgodi uliopo Ntyuka Dodoma, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (hayupo pichani) mgodini hapo Machi 22 mwaka huu.
Sehemu ya shehena ya mawe ya nakshi aina ya Graphite. Taswira hii ilichukuliwa Machi 22 mwaka huu wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (hayupo pichani) katika Mgodi uliopo Itiso wilayani Chamwino.
Ø Yachangia bilioni 7.1 mrabaha
2016/17
Ø Asema usimamizi mzuri unaweza
kukuza mchango huo kufikia bilioni 15 kwa mwaka.
Na
Veronica Simba – Dodoma
Naibu Waziri wa
Madini Doto Biteko, amesema kuwa madini ya ujenzi na viwanda yanaipatia
Serikali fedha nyingi kupita aina nyingine zote za madini yanayopatikana
nchini.
Akizungumza na
wafanyakazi wa Ofisi ya Madini Dodoma, Machi 22 mwaka huu akiwa kwenye ziara ya
kazi, Biteko alisema kuwa takwimu za makusanyo ya Serikali zinabainisha hayo.
“Mfano mwaka 2016/17,
takribani tani milioni 15.6 za madini ya ujenzi zilizochimbwa, zilizalisha
shilingi bilioni 230.6; ambapo katika hiyo, ulipatikana mrabaha wa shilingi
bilioni 7.1,” alisema.
Akifafanua zaidi,
Naibu Waziri Biteko alieleza kuwa, idadi ya wachimbaji wa dhahabu na madini
mengine nchi nzima ikijumlishwa, haiwezi kufika hata robo ya wale wanaofanya
shughuli za madini ya ujenzi nchini.
Alisema kuwa Serikali
imejipanga kuhakikisha inaongeza vituo vya madini ya ujenzi na viwanda kutoka
85 vilivyopo sasa nchi nzima hadi kufikia 174. “Nina uhakika tukiviongeza vituo
kufikia idadi hiyo, tutakusanya mrabaha wa zaidi ya shilingi bilioni 15 katika
madini hayo pekee.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...