Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mh. Antony Mavunde, ameupongeza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa jitihada unazozichukua katika kuimarisha hali ya usalama na afya katika sehemu za kazi nchini.
Mh. Mavunde alizitoa pongezi hizo alipozungumza na wafanyakazi wa OSHA katika kikao cha pili cha baraza la tatu la watumishi hao kilichofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
“Niwapongezi kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuboresha hali ya usalama na afya katika maeneo ya kazi hapa nchini. Kwakweli kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika utendaji wenu hasa katika kipindi cha hivi karibuni,” alisema Mh. Mavunde.
Aliongeza: “Kipindi cha nyuma mlikuwa mnafanya kazi zenu kama askari polisi jambo ambalo lilikuwa linawapa hofu kubwa wadau wenu ambao badala ya kuuelewa wajibu wao kisheria na kuutekeleza, waliishia kuwakwepa na kuwalalamikia.”
Kiongozi huyo wa serikali alieleza kwamba kwasasa watumishi wa OSHA wamekuwa wakijitahidi kufanya kazi kwa weledi mkubwa ikiwemo kuwaelimisha wadau ili waweze kuutambua wajibu wao kisheria na kuutekeleza bila kushurutishwa.
Wafanyakazi waliokingwa ipasavyo wakifanya kazi za ujenzi katika mradi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu ya kwanza ya mradi huo. OSHA huhakikisha kwamba wafanyakazi wanafanya kazi zao katika mazingira salama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...