Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Hotel ya Hyatt umemtambulisha meneja mpya wa Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar Nicolas Cedro ambaye amejizatiti katika kusaidia kuinua vipaji vya vijana hususani katika masuala ya upishi na hoteli.
Hoteli hiyo iliyopo maeneo maarufu ya Stone Town tayari imeshaweza kusaidia huduma za kijamii kama kufungua vituo viwili vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kituo cha kulea wazee wasiojiweza, elimu, maji na michezo hususani mpira wa miguu.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utambulisho huo, Nicolas Credo amesema kuwa mbali na kuwasaidia vijana katika masuala ya hoteli ambapo tayari ameshafanya mazungumzo na Waziri wa Utalii Zanzibar Mahmoud Kombo kwa ajili ya kuweza kusaidia vijana ambapo kiutalaamu yeye ana Shahada mbili za masuala ya vyakula na uendeshaji hoteli kutoka chuo kikuu cha hoteli kilichopo Nice nchini Ufaransa pia Shahada ya uzamili ya uendeshaji wa hoteli kutoka katika chuo kikuu cha E Cornel.
Cedro amesema kuwa atatumia uzoefu wa elimu, ujuzi wa lugha pamoja na ubunifu katika kujenga sifa na ubora wa hoteli hiyo na pia kwa wafanyakazi wake kwani akiwa kijana wa miaka 17 aliweza kuanza kuanza kazi ya upishi na pia anatambua umuhimu wa kuibua na kulea vipaji vya vijana na hivyo anategemea kushiriki katika shughuli za kijamii akiwa Zanzibar kwa kushirikiana na shule mbali mbali za kisiwani hapo za mapishi ili kusaidia vijana wenye vipaji vya upishi waweze kupata ujuzi wa kimataifa alio nao na hivyo waweze kujiendeleza katika fani hiyo na kuitumia kama njia ya kujiinua kiuchumi.
Meneja mpya wa Park Hyatt Zanzibar Nicolas Cedro akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa na akielezea mikakati yake ya kuinua vipaji vya vijana katika masuala ya upishi na hoteli Visiwani humo. Kushoto ni Meneja Masoko Milvas Burnice.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...