Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amewashauri Wasimamizi na waratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini( TASAF) kushirikiana na viongozi wa vijiji na wataalamu wa aridhi kuanzishisha miradi itakayokuwa endelevu ambayo itakawaondoa haraka wanufaika wa mfuko huo.

Polepole ametoa kauli hiyo jana akiwa kwenye ziara yake ya mkoani Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kutembelea wanufaika wa TASAF katika Kijijji cha Nyabitaka wilayani Kibondo mkoani Kigoma.Alipata nafasi ya Shamba darasa lenye hekari mbili la kilimo cha mseto kinachosimamiwa na wanufaika hao.

Polepole amewashauri waratibu wa TASAF kushirikiana na watalaamu wa aridhi na viongozi wa vijiji kutenga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya wanufaika badala ya kuwapatia Sh.40,000 kwa kila mwezi.

"Wasikisimamiwa vema kwenye kilimo watapiga hatua za kimaendeleo haraka zaidi na baada ya mwaka mmoja wanafuika hao hawatakuwa masikini tena.Hivyo ni vema mkaangalia mbinu sahihi za kuwaondoa wanufaika hawa kwenye umasikini,"amesema Polepole.

Amesema Serikali ya CCM imeandaa mpango huu wa maendeleo kwa ajili ya kunusuru kaya masikini na lengo ikiwa ni kuwainua watu watoke kwenye umasikini uliopitiliza na kufafanua mwaka 2025 mpango huo wa TASAF utakwisha endapo utamalizika na wananchi hawajapatiwa miradi ya kujikwamua na umasikini itakuwa haijasaidia chochote.

Amewaahidi wananchi wilayani Kibondo kuwa Serikali ya Awamu ya tano ya CCM itatoa Sh.milioni 52 kwa ajili ya wananchi wakopeshwe kwa lengo la kuwaondoa kwenye umasikini na kuwaomba watendaji na wenyeviti wa vijiji kuandaa utaratibu bora wa kuwakopesha Wananchi hao kwa utaratibu mzuri.

Kwa upande wa Mratibu wa TASAF mkoani Kigoma Jailos Pilla aMEsema utaratibu wa mfuko huo ni kuwa Wanufaika kubuni mradi wa maendeleo.Hivyo baada ya kubuni mradi na kuwezeshwa na TASAF baadae mradi unakuwa mali ya Serikali ya kijiji.

Amesema kila mnufaika anatakiwa kujifunza kupitia miradi hiyo inayoanzishwa ili aweze kuanzisha nyumbani kwake ili ajikwamue katika umasikini.Mmoja wa wanufaika wa TASAF, Lucia Mihayo amesema fedha alizozipata alizitumia kununa tofali na bati na mpaka sasa ameanza ujenzi wa nyumba ya bati ili aishi vizuri yeye na familia yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...