Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita ametemtembelea nyumbani kwakwe na kisha kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwasisi na mkongwe wa Chadema Victa Kimesela ambaye anaumwa kwa muda mrefu sasa.
Kimesela ni miongoni mwa waasisi walioshiriki kuandaa Katiba ya chama hicho mwaka 1992, anaugua kwa muda ambapo familia yake ilimueleza Meya Mwita kuwa alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na hivyo kuruhusiwa Jumatano iliyopita.
Taarifa iliyotolewa leo na Ofisa Habari wa Ofisi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam Christina Mwagala amesema muda fupi baada ya Meya Mwita kufika nyumbani kwa mwasisi huyo, afya yake ilibadilika.
Hivyo kwa kushirikiana na familia hiyo walitoa taarifa Muhimbili ili kupatiwa gari ya kubebea wa gonjwa.Aidha gari hiyo ilifika na kisha Mwita na familia hiyo waliambatana pamoja kumuwahisha kwa mara nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu awali.
Mwagala amesema kuwa Kimesela amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chadema, ikiwepo kuwa Katibu mtendaji wa chama hicho wakati wa utawala wa mzee Edwin Mtei.
Pia amewahi kuwa Katibu mkuu wa muda wakati wa utawala wa Bob Makani(marehemu)na hivyo kumuachia nafasi hiyo Dk.Wilblod Slaa ambaye kwa sasa amestaafu siasa tangu mwaka 2015.
Mstahiki
Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita akiwa pamoja na familia ya
Kimesela ,wakitoa msaada wa kumpakiza kwenye gari ya kubebea wagonjwa ya
hospital ya Taifa Muhimbili jana alipomtembelea nyumbani
kwakwe.Kimesela anaumwa na kwa sasa amelazwa katika hospital ya Taifa
Muhimbili.
Mstahiki
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na mke wa
Kimesela , Suzani Kimesela alipomtembekea nyumbani kwake jana .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...