Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akionesha kitabu cha
vyeti vya kuzaliwa pamoja na simu ya kisasa alipozindua zoezi la usajili
na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na
Simiyu. Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha
zoezi hill. Kulia ni Mwenyekiti was Bodi ya RITA, Prof. Hamisi Dihenga.
MARA
– Mkoa wa Mara na Simiyu imezindua kuanza kwa mfumo wa kujitegemea wa
usajili wa vizazi ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watoto 700,000
walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo.
Uzinduzi
huo uliofanyika katika mji wa Musoma, ulihudhuriwa na Mheshimiwa Waziwa
wa Katiba na Kisheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi,
UNICEF na Mwakilishi wa Serikali ya Canada na wageni wengine mashuhuri.
Mfumo huo wa usajili uliorahisishwa utasaidia usajili wa watoto wote
wachanga na kupunguza idadi kubwa ya watoto ambao hawajasajiliwa walioko
chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo miwili.
Mfumo
huu ambao unajitegemea usio ratibiwa kutoka serikali kuu unasogeza
huduma ya usajili karibu na jamii. Inaanzisha vituo vya usajili katika
vituo vya afya, ambavyo vinatoa huduma ya afya ya uzazi na watoto, na
kwenye jamii katika ofisi za mtendaji wa kata kuendana na sera ya
serikali ya ugawaji wa madaraka kwa serikali mitaa.
Zoezi
hili limeziba pengo la mijini na vijijini, kwa kuzipa jamii za
pembezoni nafasi ya kusajili watoto wao. Inatatua suala la msingi la
upatikanaji na uwezo wa kumudu jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa
katika usajili wa vizazi nchini Tanzania.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...