Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

SERIKALI imetoa tahadhari kwa watumishi ,wakandarasi na wadau wa sekta ya Nishati wanao husika na miradi wasitikise kiberiti kwa kuhamasisha maandamano kupitia shida za wananchi.

Aidha wizara ya Nishati imesema itatumia kiasi cha shilingi trilioni sita kwa ajili ya kuyafikia maeneo 7,873 nchi nzima ili yaunganishwe na huduma ya umeme kupitia miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Hayo yalisemwa kwenye mtaa wa Sagale Magengeni kata ya Viziwaziwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akitembelea maeneo yaliyoko kwenye miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Alisema kuwa ole wake anayetumia tumia shida za wananchi kuhamasisha maandamano kwani akibainika chamoto atakiona.Mgalu alieleza hayo baada ya kauli ya mwananchi mmoja ambaye alikuwa akitaka umeme na kuambiwa kama anataka umeme aandamane maandamano ya Mange Kimambi.

“Serikali imeshtushwa tena inatokea maeneo haya kwa watu waliopewa dhamana mkandarasi ni dhamana huwezi kuleta jeuri kama unazo fedha usingeomba kazi hizi ni fedha za Rais Dk. Magufuli usilete jeuri,” alisema Mgalu.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka na Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu wakibonyeza kiwashio ikiwa ni sehemu ya kuuwasha umeme umeme mtaa wa Mbwawa Mkoleni,wilayani Kibaha.Picha na Mwamvua Mwinyi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...