Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga na Uongozaji Ndege (CANSO)akichukua wadhifa huo kutoka kwa Thabani Mthiyane wa Afrika Kusini aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka sita.
Bwana Johari ambaye atakuwa kwenye wadhifa huo kwa miaka mitatu, amechanguliwa tarehe 5 Machi 2018 katika mkutano wa CANSO unaofanyika Madrid Hispania na anatarajiwa kuthibitishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wa CANSO uliopangwa kufanyika mwezi Juni Bangkok, Thailand. Kutokana na uteuzi huo, Bwana Johari anakuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya CANSO (EXCOM) ambacho ndicho chombo cha juu cha usimamizi wa shughuli za shirikisho hilo. Bwana Mthiyane anatarajiwa kukabidhi majukumu ya mwenyekiti wa CANSO Afrika kwa Johari baina ya mwezi Machi na Juni 2018.
Tunapenda kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TCAA na kumtakia mafanikio katika majukumu haya mapya CANSO ni Shirikisho la Kimataifa la Huduma za Anga na Uongozaji Ndege za Kiraia Duniani. Wanachama wa CANSO wanatoa huduma hizo kwa asilimia 85 kote duniani. Wanachama wa shirikisho wanabadilishana taarifa na kuandaa sera zinazolenga kuboresha huduma za anga na uongozaji ndege.
IMETOLEWA NA OFISI YA HABARI MAMLAKA YA USAIFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...