Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii
HALI ya taharuki imeibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutokea kwa mlipuko wa moto uliosababishwa na Transfoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji wa Mahakama hiyo, Gasto Kanyairita amesema moto huo umetokea saa nne asubuhi.
Amesema wakati mlipuko huo unatokea kulikuwa na kesi nyingi zikiendelea mahakamani.

"Baada ya kufuatilia tulibaini kuwa ni transformer ambapo ilisababisha kuungua kwa waya wa TTCL, simu na Internet ambapo shughuli za Mahakama zilisitishwa kwa muda," amesema.

Pia amesema shughuli za Mahakama zinaendelea ambapo data za kesi zipo salama.
"Niwatoe hofu Watanzania mlipuko uliotokea ni wa shoti ya umeme na ni kawaida kutokea, hivyo waepukane na taarifa za uongo,"amesema.


Mmoja wa mashuhuda tukio hilo, amebainisha kuwa walisikia kishindo kikubwa cha mlipuko ambapo iliwabidi wakimbizane kutoka nje ya Mahakama.

"Ilitubidi tutoke nje kutokana na hofu tuliyokuwa nayo, lakini tunashukuru hakuna madhara yoyote ya kibinadamu,".
 Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Gasto Kanyairita, akifafanua juu ya mlipuko uliotokea leo asubuhi na kusababisha taharuki kwa wananchi waliokuwepo mahakamani hapo.
Wananchi mbali mbali wakitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusikia mlipuko wa moto ndani ya mahakama uliosababishwa na Transformer.

 Gari la zimamoto likiwa limefika eneo la tukio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...