Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salimu ASAS ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Iringa Mjini kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi. 

Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Iringa Mjini mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo Iringa Mjini na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati na Rose Tweve 

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya Iringa Mjini kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas 
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akiongea na wajumbe wa baraza la UWT manispaa ya Iringa lilofanyika katika ukumbi wa CCM sabasaba na kutoa jumla ya shilingi milioni kumi na tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akipokea zawadi kutoka kwa viongozi wa UWT manispaa ya Iringa
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akibadilisha mawazo na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...