Na Yusuph Mussa, Korogwe.
BWENI la Mapinduzi la wanafunzi wa kidato cha pili na nne katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe limeteketea kwa moto, huku mali zote za wanafunzi ikiwemo fedha zimeungua.
Moto huo ulioanza 3.15 usiku jana Machi 4, 2018, uliwakuta wanafunzi 43 wa bweni hilo wote wakiwa darasani (prepo), hivyo mali zao zote kuanzia vitanda 19 vya kulala wanafunzi wawili wawili na vitanda vitano vya kulala mtu mmoja vimeteketea kwa moto.
Akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela, Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Rehema Bwasi, alisema mali nyingine zilizoteketea ni magodoro 43, ambapo kati yao 26 ni ya shule na 17 ya wanafunzi. Pia vyandarua 43, shuka 86, blanketi 43, masanduku ya bati 43, mabegi 43 na fedha taslimu za wanafunzi mmoja mmoja sh. 336,500.
"Vitu vingine vilivyoungua ni pamoja na nguo za wanafunzi, miswaki, sabuni, vikombe, sahani pamoja na vitabu vya wanafunzi na vya shule. Ila tathmini inaendelea ili kuweza kujua hasara iliyotokana na moto huo" alisema.
Bwasi alisema kutokana na kadhia hiyo, baadhi ya wanafunzi walipata mshtuko, huku wengine wakiwa na magonjwa mbalimbali kama pumu na kifua, hivyo wanafunzi 41 walipelekwa Hospitali ya Wilaya na saba Zahanati ya Majengo.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Machi 5, 2018 alifika Wilaya ya Korogwe kuangalia athari za moto Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe. Pichani akimfariji mmoja wa wanafunzi waliopata mkasa wa kuunguliwa na bweni la shule hiyo. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela leo Machi 5, 2018 alifika Wilaya ya Korogwe kuangalia athari za moto Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe. Pichani akimfariji mmoja wa wanafunzi waliopata mkasa wa kuunguliwa na bweni la shule hiyo. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said.
Bweni la Mapinduzi la Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe ambalo limeteketea kabisa kwa moto jana usiku Machi 4, 2018. Bweni hilo walikuwa wanalala wanafunzi 43 wa kidato cha pili na nne.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...