Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayoongoza kwa kutoa huduma bora za smartphone leo imetangaza uhuru wa mawasiliano kwa kuzindua huduma kabambe ya kipekee kwa wateja wake wanaopiga simu na kutuma sms kwenda mitandao yote nchini. 

Taarifa iliyotolewa na Airtel leo imesema bando za uhuru zinakuja baada ya serikali hivi karibuni kuweka punguzo kubwa la gharama za kuunganisha simu zinazokwenda mitandao mingine (interconnection rate) na hivyo Airtel kuona vyema kuwapa wateja wake fursa ya kufurahia punguzo hilo kupitia huduma yake itakayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Wateja wote watapiga na kutuma sms mtandao wowote nchini baada ya kujinunulia bando nafuu ya shilingi 1000 au bando mpya ya shilingi 600 tu.

 ‘Yatosha Mitandao Yote’ ni bando bora kuliko zote nchini zinazowawezesha wateja wa Airtel kujipatia vifurushi vyenye muda wa maongezi mara mbili zaidi ya  ilivyokuwa awali. Mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24, hapo awali kifurushi hiki cha shilingi 1000 mteja alipata dakika 25 tu. 

Vilevile kwa kifurushi kipya kimeongezwa faida ili kumpa mteja dakika 16, 2MB na 50 sms  kwenda mitando yote kwa shilingi 600 tu. Zaidi ya hapo wataendelea kujipatia vifurushi nafuu kwa SIKU, WIKI, MWEZI kwa kujiunga baada ya kununua vocha kwa kupiga *149*99# kisha chagua YATOSHA MITANDAO YOTE au kujiunga kupitia huduma ya Airtel Money na kufurahia Uhuru wa kuongea.

Akiongea jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzindua wa Yatosha Mitandao Yote, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kuwa “wateja wanabaki kuwa ndio nguzo kuu yetu kwenye biashara, ni furaha kubwa kwetu kuzindua huduma ya Yatosha Mitandao Yote ambayo itawapa wateja wa Airtel unafuu zaidi na uhuru  wa kutumia huduma za mawasiliano. Tunaendelea kufanya utafiti kufahamu mahitaji ya wateja pamoja na kuongeza ubunifu ili kuleta huduma nafuu zaidi ”
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania, Sunil Colaso(katikati), Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano(kulia) na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon, wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Sunil Colaso.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...