Wananchi
wa mtaa wa Tungwi-Songani Kata ya Pembamnazi Manispaa ya Kigamboni
wametakiwa kutunza miundombinu ya soko ili soko liweze kudumu kwa muda
mrefu na kunufaisha wananchi wote kwa ujumla.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni
Mh.Maabadi Hoja alipokuwa akizindua mradi wa soko hilo ijumaa
lililojengwa Mtaa wa Tundwi-Songani , alisema kuwa mradi huu umenza
ujenzi muda mrefu tangu mwaka 2002, hivyo tunatarajia ukamilikaji wake
utaleta maendeleo kwa wananchi wote wa Tundwi Songani na jamii nzima ya
Kata ya PembaMnazi hivyo ni muhimu kuhakikisha unatunzwa.
Alisema
kuwa ulinzi uimarishwe wa miundombinu na kuhakikisha lengo
lililokusudiwa la kuboresha mazingira na utoaji wa huduma kwa
wafanyabiashara na wananchi wa Tundwi na kata ya Pemba Mnazi kwa ujumla
linafikiwa.
Akitoa
taarifa ya mradi Mratibu wa TASAF Manispaa ya kigamboni Bi.Janet
Kacholi alisema kuwa, mradi wa soko ni miongoni mwa miradi iliyoibuliwa
na wananchi kupitia program ya TASAF, ambapo umelenga kutoa ajira kwa
vijana kwa kupata fursa ya kuuza mazao mbalimbali na kuiwezesha Serikali
kupitia Halmashauri kukusanya mapato kutokana na ushuru mbalimbali
utakaotozwa kwa wafanyabiashara.
Aliongeza
kuwa hadi kukamilika kwa ujenzi wa soko hilo jumla ya Tsh.91,858,842.24
zimetumika ambapo wananchi wamechanga kiasi cha Tsh.34.040.427.27
mchango wa TASAF ni Tsh.26,416,827.27 na Halmashauri ya Manispa ya
kigamboni imetoa Tsh.31,401,587.7 ambazo zimekamilisha ujenzi wa meza za
ndani baada ya Halmshauri ya Temeke kushindwa kutoa fedha za
ukamilishaji kama ilivyoahidi wakati wa uibuaji wa mradi kabla ya
kugawanywa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya kigamboni Mh. Maabadi Hoja akifungua kitambaa cha jiwe la msingi kuonesha uzinduzi rasmi wa soko
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Kigamboni Bi. Janet Kacholi akisoma taarifa ya mradi kabla ya uzinduzi.
Mstahiki Meya akiwa ameongozana na wananchi wakikagua soko mara baada ya uzinduzi.
muonekano wa soko kwa nje
Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa soko.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Kigamboni Bi. Janet Kacholi akisoma taarifa ya mradi kabla ya uzinduzi.
Mstahiki Meya akiwa ameongozana na wananchi wakikagua soko mara baada ya uzinduzi.
muonekano wa soko kwa nje
Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa soko.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...