TAASISI ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), imepongezwa kwa kazi zake inazofanya za utafiti na kutoa mwelekeo sahihi wa uanazuoni kwenye masuala mazito yanayotakiwa kutekelezwa na wananchi wa Tanzania kuendeleza ustawi na kuinua uchumi.
Aidha imepongezwa kwa kurejea kuipitia sera ya maendeleo endelevu (SIDP) ya mwaka 1996 ambayo kwa sasa inahitaji kufanyiwa marekebisho kuendena na maizngira ya sasa.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Elisante Ole Gabriel, katika hotuba iliyosomwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara hiyo, Obadiah Nyagiro wakati akifungua mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara?
Alisema kwamba majadiliano hayo yanakwenda sawa na juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kujikita katika maendeleo ya viwanda ambapo uwekezaji na biashara ni vitu muhimu.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Obadiah Nyagiro akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa tano wa wajumbe
wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu
yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu
ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na
biashara? kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof Elisante Ole
Gabriel uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam
Mkuu
wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa
niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dk. Tausi Kida wakati wa
mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera
na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya
maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali
ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF
jijini Dar es Salaam.
Mtafiti
mshiriki wa ESRF Prof. Samwel Wangwe, akiwasilisha mada kuhusu
mapendekezo ya vigezo vya kuipitia upya sera ya maendeleo endelevu
wakati wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa
kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo
walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama
wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti
wa Huru wa masuala ya Jinsia na Maendeleo Prof. Marjorie Mbilinyi
akichangia hoja wa mkutano wa tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo
wataalamu wa kupitia sera na maeneo maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5)
ambapo walijadili sera ya maendeleo endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya
usalama wa chakula, hali ya hewa na biashara? uliofanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Msajili
wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano akichangia mawazo wakati wa mkutano wa
tano wa wajumbe wa kitaifa wakiwemo wataalamu wa kupitia sera na maeneo
maalumu yanayogusa maendeleo (NRG5) ambapo walijadili sera ya maendeleo
endelevu ya viwanda: Nini Nafasi ya usalama wa chakula, hali ya hewa na
biashara? uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Obadiah Nyagiro (katikati) na Mkuu wa
Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...