Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewaagiza wahifadhi wote nchini kuhakikisha kuwa hakuna misitu inayoendelea kuharibiwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa elimu kwa wananchi wanaozunguka misitu ya hifadhi ili wasiweze kukata miti ovyo kwa ajili ya makazi na shughuli za kilimo
Ametoa agizo hilo Machi 24, 2018 katika Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wakati akifunga mafunzo ya kwanza kwa Wakala ya Huduma za Misitu (TFS) ya mabadiliko ya kuelekea mfumo wa Jeshi Usu kwa Maafisa na viongozi 108 wa TFS na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.
“Misitu yetu inaendelea kuharibiwa kutokana na baadhi ya watu kuendesha shughuli za kibinadamu katika maeneo ya hifadhi kama vile uchimbaji madini usiozingati taratibu, uchomaji misitu kwa ajili ya kuandaa mashamba pamoja na kilimo cha kuhama hama.’’Kazi ya ulinzi wa rasilimali zetu za asili ni yetu na tusikubali hali hii iweze kuendelea,,” alisema Waziri Hasunga
Aidha, alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo kuingiza mifugo, kuanzisha kilimo, makazi na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na matumizi mengineyo.
Awali akizungumzia mafunzo hayo alisema, lengo ni kubadilisha utendaji katika sekta ya uhifadhi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu ambao utaongeza nidhamu, uwajibikaji, uadilifu na maadili kwa watumishi wote wa sekta hiyo ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili za taifa.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua gwaride la
Maafisa wa Misitu na Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa huduma za Misitu
Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro muda mfupi kabla ya
kuwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu katika kituo cha
Mlele mkoani Katavi.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto )
akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya jeshi Usu, Mkurugenzi wa
Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu za Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) Mohamed Kilongo katika kituo cha Mlele mkoani
Katavi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Lilian Matangi, wa
kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof, Dos Santos Silayo pamoja na
Tutubi Mangazeni.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wahitimu
wa Jeshi Usu wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo jana mkoani Katavi.

Baadhi
ya Maafisa wa Misitu na Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa huduma za
Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro wakimsikiliza,
Naibu Waziri Japhet Hasunga muda mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya
kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akipokea salamu za Jeshi Usu wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Baadhi
ya Maafisa wa Misitu na Wanyamapori 108 kutoka Wakala wa hudum za
Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Eneo la Ngorongoro wakila kiapo muda
mfupi kabla ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Jeshi Usu jana
katika kituo cha Mlele mkoani Katavi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...