Na Bashir Yakub
1. HATIMILIKI YA KIMILA NI IPI.
Hati ya ardhi ya kimila ni nyaraka ya umiliki wa ardhi ambayo inatoa utambuzi maalum wa umiliki wa ardhi. Hizi ni sawa na hati miliki zile mnazozijua ambazo hutolewa kwa ardhi za mijini japo ipo tofauti kidogo. Moja ya tofauti ya hati ya kimila na hatimiliki za mijini ni kuwa hizi husimamia ardhi mijini wakati hizi nyingine husimamia ardhi za vijijini.
2. HATI YA KIMILA HUTOLEWA NA NANI.
Hati ya umiliki wa ardhi ya kimila hutolewa na baraza la ardhi la kijiji( land village council). Kila kijiji kinalo baraza hili. Pia baraza hili ndilo linalowajibika kwa masuala ya kila siku ya ardhi ya kijiji. Kwa hiyo maombi yote ya kuomba ardhi au hati ya kimila yataelekezwa baraza hili.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...