Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Francophonioe
ambayo itaanza Machi 18 hadi Machi 25, Balozi wa Ufaransa nchini
Frederic Clavier amesema katika nchi hizo kuna nafasi za kazi nyingi
ambazo kama Watanzania watajifunza Kifaransa wanaweza kuzipata.
Alisema
Tanzania inazungukwa na nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa kama
Burundi, Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na hivyo kwa
wananchi wa Tanzania hiyo ni fursa ambayo wanaweza kuitumia katika
shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.
"Hapa
Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili
linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa
wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu
waitumie."
"Tanzania
inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni
muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya
Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza
Kifaransa," alisema Clavier.
Aidha,
Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania
kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF
ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française,
Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo
Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...