Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi na Viongozi Mkoani humo kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wataalam wa Takwimu katika utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi unaoendelea hapa nchini ili kuwezesha upatikanaji wa  takwimu halisi na sahihi Mkoani humo.

Mtaka ameyasema hayo katika Mkutano wake na   waandishi wa habari, wataalam wa Takwimu na Viongozi wa madhehebu ya dini uliofanyika Februari 28 Mjini Bariadi.

Amesema Utafiti huo utatoa makadirio ya uchumi jumla(macroeconomic), hususani matumizi ya kaya kwa ajili ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product-GDP), kupata mwenendo wa matumizi ya moja kwa moja ya kaya  ili kuwezesha uchambuzi wa hali ya soko na kupata taarifa za umilikaji wa vifaa vya kudumu pamoja na nyenzo za uzalishaji wa kipato.

Amesema kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2015 kila mwananchi anawajibika kushiriki katika utafiti kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu rasmi ambazo zitatumika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika Ofisini kwake Mjini Bariadi.
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donatus Weginah akifafanua jambo katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.
 Meneja wa Takwimu, Mkoa wa Simiyu, Ndg.Nestory Mazinza akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...