SERIKALI  ya Mkoani Tabora imesema kuanzia msimu ujao mazao yote ni lazima yalimwe kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora kinachosisitiza matumizi ya mbolea na ujazaji wa mazao kitaaalamu ili kuhakikisha kunakuwa na mavuno mengi ambayo yatawawezesha wakulima kuzalisha ziada ambayo itawasaidia kuwaletea maendeleo yao binafsi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Kaliua na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiendelea na  kampeni zake za kuelimisha wakulima wa pamba juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu waharibifu katika pamba.

Alisema ulimaji wa hivi sasa kwa  wakulima walio wengi hauzingatii ujazaji wa miche(plant population) kitaalamu katika mashamba yao na matumizi ya mbolea jambo linalopelekea kuwepo na mavuno machache katika eneo kubwa shamba hatua ambayo inamfanya mkulima kuwa na mavuno machache.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kilimo kijacho ni lazima wakulima wote waliopo  Mkoani Tabora walime kilimo kinachowasaidia kuzalisha ziada na kupata fedha kwa ajili ya kupanua kilimo chake na kuboresha maisha yao.

"Kuanzia sasa ni marufuku kwa wakulima kwa Mkoa huu kulima zao lolote iwe mchicha, viazi , mahindi na mazao ya biashara bila kufuata mistari na kujaza mazao katika shamba...siwezi kuendelea kuvumilia wakulima wanaendelea kulima kilimo ambacho hakiwasaidia kupiga hatua na kuondokana na umaskini kwa kuzalisha mazao mengi katika eneo dogo" alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga( wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kulia) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Mratibu wa Pamba wa Wilaya ya Kaliua Samwel Mushi(kushoto) na Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage(kulia).
 Mshauri wa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Modest Kaijage(kulia)  akitoa maelezo jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kulia) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga(kushoto) na Afisa Tarafa ya Kaliua Bethod Mahenge (wa pili kulia)
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kushoto) akizungumza jambo jana kwa Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga( kushoto) wakati alipotembelea shamba la pamba la Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha wakulima wa zao juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu. Wengine ni Afisa Tarafa ya Kaliua Bethod Mahenge(wa pili kulia) na Mshauri wa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage(kushoto). Picha na Tiganya Vincent
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...