Serikali kupitia, Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), imetekeleza maombi 5 ambayo yanawasaidia wafugaji hao  kuongeza thamani ya mifugo yao  kupitia Soko la Kimkakati la mifugo Longido lililojengwa na Program hiyo.

Mwishoni mwa mwaka 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama, alikuwa na ziara ya kukagua  ujenzi wa soko hilo wilayani humo, ambapo  baada ya ukaguzi alikutana na wafanyabiashara ya mifugo, ambao  waliwasilisha maombi  5,  ambayo yangeweza kuongeza Thamani Biashara za Mifugo na kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo.

“Serikali ya awamu ya tano imeamua kuwasikiliza watu wanyonge na ambao wanajituma kuchapa kazi, lakini pia lengo la Program ya MIVARF ni kuongeza kipato kwa  wananchi hasa waishio vijijini, kwa mantiki hiyo nilimuelekeza Mratibu wa Program Kutekeleza maombi yao haraka sana ili wafugaji hawa wapate tija ya ufugaji kupitia soko hili” alisema Mhagama

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Mifugo wilayani Longido, Saruni Laizer amesema maombi waliyowasilisha serikalini ili waweze kupata tija ya mifugo kupitia soko la Kimkakati la Mifugo Longido yamefanyiwa kazi na Program ya MIVARF ndani ya miezi mitatu tangu wayasilishe, ikiwa ni; Mizani ya kupima mifugo, Maji ya kunyweshea mifugo, machinjio, Josho, pamoja na  umeme.

“Tulihitaji maji hapa ili mifugo isije ikafa wakati inasubiri kuuzwa kwa kukosa maji, lakini umeme hapa ni muhimu kwani biashara zetu zinafanyika usiku, tayari hadi jenereta imeletwa kwa ajili ya kuhakikisha biashara haikwami kwa dharura yoyote ile, lakini mizani itasaidia kutowauza mifugo kwa kuangalia kwa macho bali kwa uzito wao” alisema Laizer
 Sehemu ya kunyweshea mifugo iliyojengwa katika ​​Soko la Kimkakati la Longido,  Wilayani Longido kwa ufadhili wa  Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Baadhi ya mifugo wakiwa katika eneo la kunywa maji kablaya kuuzwa katika Soko la Kimkakati la Longido,  Wilayani Longido ambalo limejengwa kwa  ufadhili wa  Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...