Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Wanawake
wanaweza kuleta mabadiliko ya maendeleo katika jamii ikiwa watasimama
imara kwa pamoja na kuwezesha wenzao ambao hawana elimu ya kutosha. Hayo
yamesemwa na mapema leo Machi 10, 2018 na Meneja wa Udhibiti na Sayansi
wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi wakati akizungumza
katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani
yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa wanawake wanaweza kufanya mabadiliko kwa kila mmoja kuwa imara na
kuamsha wanawake wengine ambao hawajafikiwa na fursa zikiwemo cha uchumi
au za ubunifu za kuweza Marsha amasema kuwa kuadhimisha siku ya
wanawake lazima kulete mabadiliko sio kuadhimisha tu halafu hakuna
matokeo chanya yanayoonekana kwa wanawake tutakuwa hatujatenda haki
katika kujipambanua ili kuweza kufikia malengo kwa wale wale
walioasisi.
Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa Soaring Women International, Luphurise Lema amesema
kuwa wakati alipokuwa anafanya kazi aliona kuwa watu waliosoma nje ya
ndio wana akili lakini alitambua kuwa sio hivyo tofauti yake ni
kujiamini tu na kuamini kila kinachofanyika hata mwanamke anaweza.
Luphurise amesema kuwa kila mwanamke asimame imara na kuamini kila
anachofanya anaweza kuleta mabadiliko hata ya dunia.
Nae
mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri Ali Masoud ‘Masoud
Kipanya’ ambaye ni mchora katuni na mtangazaji wa Cloud Radio/Tv ja ya
Watengeneza mjadala, Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ amesema kuwa wanawake
ni watu muhimu na majukumu anayofanya mwanamke akipewa mwanaume hawezi
kuyafanya isipokuwa alioanzisha kauli kuwa hawawezi ndio imewafikisha
wanawake lakini wakaze buti wanaweza kuleta mabadiliko.
Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha
Macatta-Yambi akizungumza wakati wa mkutano wa kilele cha maadhimisho ya
siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women
International iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soaring Women International, Luphurise Lema akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2018 aliyoandaa jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (katikati) akiwa katika moja waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke katika maadhimisho ya siku wanawake Duniani leo jijini Dar es Salaam. Kutoka ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura, na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soaring Women International, Luphurise Lema (kushoto).

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura (katikati) akichangia mada ya nafasi ya mwanamke katika jamii katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mchoraji wa Katuni na Mtangazaji wa Clouds Radio/TV, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (kushoto) na Mratibu wa UN Global Compact Network Tanzania, Emmanuel Nnko (kulia) na Dk. Florence Temu kutoka AMREF (wa kwanza kulia).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...