Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, mwaka huu shirika hilo itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao Government e-Payment Gateway (GePG).

Imesema mfumo utaanza kutumika kutokana na matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya Tanesco makao makuu imesema shirika hilo ni miongoni mwa Taasisi za Serikali,hivyo itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi zake.

Pia Kampuni za simu pamoja na benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki. 

"Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa Tanesco itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike Tanesco ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio.

" Baadhi ya taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji. Tunapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka,"imesema taarifa hiyo.

Ufafanuzi huo wa Tanesco unakuja baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo inadai mkataba kati ya Tanesco na Maxcom(MaxMalipo)wa kuuza token za umeme utakwisha mwisho mwa nwezi huu na hakuna dalili wataongezewa mkataba.

Taarifa hiyo ikadai kutokana na hali hiyo ni vema wateja wakachukua tahadhari kwani baada ya Machi 31anayetaka kununua umeme itabidi aende ofisi za Tanesco.

Hivyo Tanesco wameamua kufafanua kuhusu mfumo mpya ambao utatumika wateja kununua umeme na kuwahakikishia wataendelea kununu kama zamani na hakutakuwa na tatizo lolote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...