Na
Bashir Yakub.
Bubu yaani mtu asiyeweza kuongea anaweza kuwa shahidi mahakamani iwapo
ameshuhudia tukio. Kutokuwa na uwezo wa kuongea hakumwondolei sifa ya
kushuhudisha kile ambacho amekishuhudia.
Ikumbukwe ushuhuda unatokana na na hatua ya mtu kuona, kusikia, kuhisi,
kugusa, au utambuzi wa tukio kwa namna
yoyote ambao umetokana na kiungo cha
mshuhudiaji.
Yumkini, bubu wengi hawasikii. Na tumeona hapo juu kuwa
ushuhuda ni pamoja na kusikia. Hata hivyo pamoja na kutosikia kwao bado wanavyo
viungo vingine vya mwili ambavyo wanaweza kuvitumia kushuhudia tukio. Viungo
hivyo ni pamoja na macho, mikono kugusa, ulimi kuhisi,akili katika utambuzi nk.
1. SHERIA KUHUSU BUBU SHAHIDI.
Kifungu cha 128( 1 )
cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 kinasema kuwa mtu ambaye
hawezi kuongea(bubu) anaweza kutoa
ushahidi wake katika namna
nyingine ambayo itaweza kuwa fanisi na ya kueleweka. Njia fanisi na ya kueleweka ni kama kupitia
maandishi/kuandika ikiwa anao uwezo wa kuandika, na kwa ishara ikiwa anao uwezo
wa kutumia ishara.Wengi tunajua ishara kama njia kuu ya mawasiliano kwa bubu.
Basi hiyohiyo inaweza kutumika kwa bubu kutoa ushahidi.
2. HALI IKOJE KAMA HAKIMU/JAJI HAELEWI ISHARA YA BUBU.
Bubu anapotoa ushahidi wake kwa ishara panatakiwa pawepo mtu
ambaye atatafsiri ishara zile kwa maneno. Hata kamaHakimu/Jaji angekuwa na
uwezo wa kujua ishara za bubu bado mtu anayetafsiri anatakiwa kuwepo. Hii ni
kwasababu mahakamani hayupo hakimu tu. Bali wapo wapo wengine kama upande wa mashtaka
, upande wa utetezi ambao wangependa kujua nini bubu anaongea katika ishara
zake ili wapate kumuhoji na kumuuliza maswali kuhusu kile alichoongea.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...