Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Mwenyekiti
wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wametembelea eneo la
Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika
eneo la Njedengwa mkoani Dodoma.
Mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi na kukagua maendeleo ya
ujenzi wa jengo hilo wajumbe hao wameonyesha kutoridhishwa na kasi ya
ujenzi ya Wakala wa Majengo nchini Tanzania (TBA) wanaojenga jengo
hilo na kuwataka waukamilishe mradi huo kwa wakati kama ilivyopangwa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...